• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kuuza umeme DRC

    (GMT+08:00) 2017-08-15 19:12:38
    Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimesaini makubaliano ambapo Uganda itauzia DRC umeme ndani ya miaka 3 ijayo.

    Makubaliano hayo yametiwa saini na waziri wa kawi nchini Uganda Irene Muloni na umeme huo kutoka Uganda utasambazwa kwenye maeneo ya Mashariki mwa DR Congo.

    Baadhi ya maeneo yatakayofaidika na umeme huo ni pamoja na miji ya Beni,

    Butembo na Bunia.

    waziri Muloni anasema pindi tu miradi ya kawi ya Karuma na Isimba itakapokamilika Uganda itakuwa na umeme wa ziada wa kuuza nje.

    Aidha alisema sasa serikali iko kwenye harakati za kuunganisha asilimia 80 ya waganda na umeme.

    Mabwawa ya Karuma na Isimba yanatarajiwa kuzalisha megawati 783 kuongezea megawati 825 zilizopo kwa sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako