• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Eneo la maonyesho ya nanenane litamegwa kwa ajili ya kuanzisha viwanda

    (GMT+08:00) 2017-08-15 19:18:26
    Eneo la maonyesho ya nanenane lililopo Nzuguni nje kidogo ya mjini wa Dodoma litamegwa kwa ajili ya kuanzisha viwanda.

    Uamuzi huo umetangazwa leo Jumanne na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jodarn Rugimbana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

    Jodarn amesema wanatenga eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya viwanda na litakalobakia litatengenezwa uwe uwanja wa kimataifa.

    Amesema katika maonyesho yaliyomalizika wiki iliyopita ambayo yamesimamiwa na mkoa baada ya kuondolewa kwenye usimamizi wa Chama cha wakulima (Taso) wamefanikiwa kukusanya Sh 226 milioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako