• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Meli ya utafiti wa sayansi ya China yagundua mnyama aina ya sponji anayesifiwa kuwa alama ya "upendo wa kudumu"

    (GMT+08:00) 2017-08-16 18:06:33

    Meli ya utafiti wa sayansi ya China tarehe 14 imefanya uchunguzi kuhusu mlima Caroline ulioko chini ya eneo la magharibi la bahari ya Pasifiki ambao binadamu hawajawahi kuuchunguza, na imekusanya sampuli nyingi za viumbe na jiografia, ikiwemo mnyama aina ya sponji wa rangi ya njano ambaye ni nadra kugunduliwa na sponji aina ya Venus's flower basket ambaye alisifiwa kuwa alama ya "upendo wa kudumu".

    Sponji ni myama wa asili zaidi mwenye seli nyingi, hana mdomo na tumbo, huwa na umbo linalofanana na chupa, nguzo au kikombe, na ana mashimo mengi mwilini, hivyo viumbe wengi wanapenda kuishi ndani ya sponji.

    Sampuli ya sponji wa rangi ya njano ina urefu wa sentimita 80. Watafiti wamesema sponji mkubwa wa rangi hii ni nadra kuona, na sponji wa kawaida huwa ni mweupe.

    Watafiti pia wamegundua sponji aina ya Venus's flower basket. Kamba aina ya Spongicola jike na dume wanapokuwa wadogo, huingia mwilini mwa sponji kupitia kwenye tundu zake. Kuishi ndani ya sponji ni salama, na bado wanaweza kupata chakula. Baadaye kamba hao wanakua na kuwa wakubwa, hawawezi kutoka tena. Dume na jike wanaishi huko maishani yao yote. Hivyo watu wa baadhi ya nchi wanawachukulia sponji wa aina hiyo kama alama ya "upendo wa kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako