• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatarajia idadi ya watalii kuongezeka kwa asilimia 20

    (GMT+08:00) 2017-08-16 19:18:31

    Kufuatia uchaguzi wa amani wakati wa msimu wa utalii ,idadi ya watalii wanaowasili nchini Kenya inatarajiwa kuongezeka katika nusu ya pili ya mwaka na kuvuka kiwango cha milioni 1.5.

    Waziri wa Utalii Najib Balala jana alitabiri ongezeko la asilimia 20 kwa idadi ya watalii mwaka huu,huku watalii wakitumia fursa hiyo kujionea uhamiaji wa nyumbu wa kila mwaka katika mbuga ya Maasai Mara.

    Hii inamaanisha kuwa serikali inalenga ujio wa watalii 1,668,000 ,ambapo ni kiwango kidogo ikilinganishwa na idadi ya watalii 1,710,800 ambao walizuru Kenya mwaka 2012.

    Idadi ya watalii kwa kawaida hushuka wakati wa uchaguzi,kwa sababu ya hofu ya ghasia kama zile zilizoshuhudiwa mwaka 2008 baada ya uchaguzi ambapo watu 1,200 walipoteza maisha yao.

    Hoteli nyingi katika ukanda wa pwani zina watalii kati ya asilimia 40-50,ambayo ni ndogo kuliko ile ya kawaida ya asilimia 60-70 wakati wa msimu wa utalii ambao unaanza Julai na kuisha Oktoba.

    Idadi ya watalii wa kimataifa iliongezeka hadi 358,985 kutoka Januari hadi Mei,ikiwa ni ongezeko kutoka 324, 276 katika kipindi kama hicho mwaka jana,ikiashiria ukuaji wa asilimia 10.7.

    Ukuaji wa haraka unatarajiwa katika nusu ya pili ya mwaka ambao utaongeza idadi ya watalii hadi asilimia 20 inayolengwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako