• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazalishaji wa ndani wajizatiti kupenyeza katika soko la EAC

    (GMT+08:00) 2017-08-16 19:19:04
    Takwimu zinaonyesha biashara kati ya Uganda na mataifa mengine ya Afrika Mashariki imeongezeka.

    Kulingana na takwimu za wizara ya Biashara,mauzo ya nje ya Uganda kwenda EAC yameongezeka kiasi kutoka $642.2 million (about Shs2.3 trillion)mwaka 2014 hadi $711.3 million (about Shs2.5 trillion) mwaka 2016.

    Uagizaji hata hivyo umepungua kutoka $684.6 million (about Shs2.4 trillion) mwaka 2014 hadi $530 million (about Shs1.9 trillion) mwaka 2016.

    Uganda huuza kahawa,majani chai na viungo.Bidhaa nyengine ambazo Uganda huza nje ni pamoja na mafuta ya kupikia,samli,sigara,chuma na nafaka.

    Bidhaa ambazo Uganda Uganda huagiza ni simiti,vifaa vya ujenzi,plastiki,mafuta,pombe,na siki.

    Wachanganuzi wanaamini kuwa iwapo hakungekuwa na vikwazo kutoka mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,viwango vya mauzo ya nje vya nchi hiyo vingeongezeka zaidi ya takwimu zinavyoonyesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako