• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msafara wa manowari za China wafika Tanzania kwa ziara ya kirafiki

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:10:45

    Msafara wa manowari za jeshi la majini la China umewasili kwenye bandari Dar es salaam Tanzania kwa ajili ya ziara ya kirafiki ya siku nne. Sherehe ya kukaribisha manowari hizo ilihudhuriwa na wachina 350 wanaoishi na kufanya kazi nchini Tanzania, na wawakili wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ.
    Akiongea kwenye sherehe hiyo, balozi wa China nchini Tanzania Bw Lu Youching, ameipongeza serikali ya Tanzania na jeshi la Tanzania kwa kuimarisha uhusiano na China.
    Katika kipindi cha siku hizo nne shughuli za mashindano yanayohusu michezo na utamaduni zitafanyika kati ya majeshi ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako