• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu za Rwanda zawasili Uganda tayari kwa mashindano ya FEASSSA

    (GMT+08:00) 2017-08-17 10:26:22
    Timu za shule kutoka Rwanda ziliondoka nyumbani kuelekea Uganda hapo jana ambapo zitawakilisha nchi yao katika mashindano ya maeneo, hii ikiwa ni toleo la 17 ya mechi za shule za sekondari maarufu kama FESSSA.

    Timu hizo 21 zilikutana katika uwanja wa IPRC- Kigali jumanne usiku ambapo walipata taarifa na kuzinduliwa rasmi tayari kwa mashindano hayo na waziri wa elimu Papias Musafiri.

    Ujumbe huo kutoka Rwanda inajumuisha watu takriban 400 wakiwemo wachezaji, makocha na maafisa wa serikali.

    Toleo la mwaka huu litafanyika kuanzia Agosti 19 hadi 27 katika uwanja wa manispaa ya Gulu iliyoko kaskazini mwa Uganda.

    Mji wa Eldoret nchini Kenya iliandaa Makala ya 16 mwaka uliopita ilihali mji wa Huye wa Rwanda ilikuwa mwenyeji wa toleo la 15. Idadi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo kutoka Rwanda zimeongezeka kutoka 17 na kufikia 21 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako