• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo lililotolewa na China linafaa kwa kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-08-17 18:08:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema kiini cha suala la nyuklia la peninsula ya Korea ni usalama, na pendekezo lililotolewa na China kwamba Korea Kaskazini inatakiwa kusimamisha majaribio ya makombora ya nyukilia, huku Marekani na Korea Kusini nazo zikitakiwa kusimamisha luteka ya kijeshi ya pamoja, ni mpango wenye haki na usawa unaoweza kutekelezwa kihalisi katika kutatua suala hilo kwa amani.

    Hivi karibuni msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Heather Neuert alipozungumzia pendekezo la China alisema mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini hauhusiani na luteka ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini, na nchi hizo mbili zitaendelea kufanya luteka hiyo. Bibi Hua Chunying amesema pendekezo la China linasaidia kutuliza hali ya wasiwasi ya hivi sasa, kutatua suala la usalama linalofuatiliwa zaidi na pande mbalimbali, na kutoa fursa ya kurejesha mazungumzo ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako