Rasi Xi Jinping alisema kwenye mkutano huo kuwa, kulinda amani, kupata maendeleo, kuhimiza ushirikiano na kutafuta mafanikio ya pamoja ni jukumu na matumaini ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, na China siku zote itoa kipauambele kuongeza ushirikiano kati yake na nchi nyingine za BRICS katika sera zake za kidiplomasia.
Mtafiti wa ngazi ya juu wa taasisi ya utafiti wa mazungumzo ya kimataifa ya Afrika Kusini Bw. Farancis Kornegay anakubaliana na maoni ya rais Xi kuhusu kujenga uhusiano wa wenzi wa kimaendeleo duniani ili kuhimiza ustawi wa pamoja, anaona uhusiano huo unaweza kupanuliwa zaidi, anasema,
"Rais Xi alitaja kuhimiza ushirikiano wa kimaendeleo duniani kote. Naona mfumo wa BRICS unaweza kubuni mkakati wa jumla, ili kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimaendeleo duniani, kwa mfano kuanzisha baraza kati ya nchi za BRICS na nchi nyingine duniani kuhusu wenzi wa kimaendeleo, ili kuziwezesha nchi zinazotaka kujiendeleza zifanya ushirikiano na nchi za BRICS."
Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa nchi za BRICS ya taasisi ya utafiti wa sayansi ya binadamu na utamaduni ya Afrika Kusini Bw. Jaya Josie anaona kuwa, mkutano wa mwaka 2013 ulifanya rais Xi afuatilie zaidi umuhimu wa Afrika, anasema
"Naona mkutano huo ulimfanya rais Xi atambue kuwa nchi za Afrika ni muhimu kwa nchi za BRICS, pia aligundua kuwa barani Afrika uchumi wa baadhi ya nchi unaendelea kwa kasi zaidi. Hivyo China imezishirikisha nchi za Afrika kwenye pendekezo lake la ukanda moja, njia moja."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |