• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania IMETISHIA KUSITISHA USAJILI WA OPARESHENI ZA UTALII ZISIZO HALALI

    (GMT+08:00) 2017-08-21 19:29:07

    Serikali ya Tanzania imetishia kusitisha kusajili oparesheni za utalii zinazoenda na kinyume na sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya utalii katika Taifa la Afrika Mashariki.

    Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Jumanne Maghembe, amesema kuwa kuna waendeshaji wa oparesheni za utalii ambayo sio waaminifu, na lengo lao kudanganya watalii wanaotaka kutembelea maeneo ya utalii nchini.

    Tanzania hupata dola bilioni 2 kila mwaka kutoka sekta ya utalii.

    Sekta hiyo inachangia asilimia 17 kwa Pato la Taifa la nchi pamoja na kutoa maelfu ya nafasi za kazi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako