• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo cha ujuzi wa maendeleo ya dunia cha China chazinduliwa

  (GMT+08:00) 2017-08-22 19:23:48

  Kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa cha China kimezinduliwa rasmi hapa Beijing, sambamba na ripoti kuhusu hatua inayopigwa na China katika kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Hizi ni hatua mbili zilizochukuliwa na China ili ya kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 iliyowekwa na Umoja wa Mataifa. Rais Xi Jinping wa China na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa walitoa salamu za pongezi.

  Mwezi Septemba mwaka 2015, mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ulipitisha ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. China ni nchi ya kwanza duniani iliyotoa ripoti husika, ambayo imejumuisha hatua na uzoefu wa China katika kuhimiza maendeleo endelevu. Kati ya malengo yote ya ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kuondoa umaskini ni muhimu zaidi. Ofisa wa ofisi ya kuwasaidia watu maskini ya baraza la serikali ya China Bw. Wu Min anasema,

  "Tangu mwaka 2013, serikali ya China imerekebisha mkakati wa kupunguza umaskini, kiwango cha watu maskini vijijini kimepungua na kuwa asilimia 4.5 kutoka asilimia 10.2."

  Mafanikio ya China katika miaka 40 yamemwachia kumbukumbu kubwa mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jorge Chediek ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya ushirikiano kati ya nchi za kusini. Anasema,

  "China imepata mafanikio makubwa katika miaka 40 iliyopita. Katika historia ya binadamu, hakuna nchi nyingine kama China ambayo iliwawezesha wananchi wake kuongeza kipato mara 20 katika miongo kadhaa. Uzoefu wa China wa kujiendeleza utakuwa mfano wenye thamani kubwa kwa dunia nzima."

  Ili kufanya utafiti kwa pamoja na kubadilishana maoni na nchi nyingine kuhusu maendeleo, rais Xi Jinping wa China alitangaza kwenye mkutano wa mwaka 2015 kuwa, China itaanzisha kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa. kituo hicho kilizinduliwa rasmi jana. Kwenye salamu zake za pongezi, rais Xi alisema anatarajia kituo hicho kitatoa mchango kwa utafiti wa mawazo ya maendeleo, kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa kwenye kazi ya maendeleo, na kuhimiza utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030.

  Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali ya China Bw. Li Wei, ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa cha China alitangaza kuwa, kituo hicho kitashughulikia kazi tatu muhimu, anasema

  "Kituo cha ujuzi wa maendeleo ya kimataifa cha China kitashughulikia kuratibu uwezo wa utafiti wa maendeleo wa China na nchi nyingine, kuendeleza mawazo na hatua halisi za maendeleo, na kuhimiza mawasiliano kati ya nchi mbalimbali duniani katika juhudi zao za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako