• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jaji wa Hispania aamua kuwapeleka gerezani washukiwa wawili wa ugaidi

  (GMT+08:00) 2017-08-23 09:54:16

  Jaji wa Hispania Bw Fernando Andreu ametoa hukumu ya kifungo kwa washukiwa wawili kati ya wanne walionusurika, kwa tuhuma za kujihusisha na mashambulizi mawili yaliyotokea wiki iliyopita nchini humo.

  Washukiwa hao wawili wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji, kujiunga na kundi la kigaidi na kumiliki vilipuzi, wametiwa mbaroni bila dhamana.

  Mshukiwa wa tatu ataendelea kushikiliwa kwa siku tatu kwa ajili ya uchunguzi zaidi, na mwingine ameachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

  Washukiwa hao wanne ni sehemu ya kundi la magaidi 12 waliojihusisha na mashambulizi yaliyotokea mjini Barcelona na Cambrils wiki iliyopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako