• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya 24 ya kimataifa ya vitabu yafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2017-08-23 18:56:07

  Maonesho ya 24 ya kimataifa ya vitabu yamefunguliwa leo hapa Beijing. Mashirika zaidi ya 2,500 kutoka nchini mbalimbali duniani yameonesha aina zaidi ya laki tatu za vitabu vilivyochapishwa hivi karibuni, na kati ya mashirika hayo, asilimia 58 yanatoka nchi za nje. 

  Maonesho ya kimataifa ya Beijing ya vitabu yamekua kwa kasi tangu yaanzishwe mwaka 1986, na hivi sasa yanachukua nafasi ya pili duniani baada ya maonesho ya vitabu ya ya Frankfurt. Mwaka huu, mashirika makubwa ya China yamepanga sehemu maalumu ya uchapisha vitabu vinavyohusu pendekezo la Ukanda moja, Njia moja. Takwimu zinaonesha kuwa, tangu mwaka 2014, biashara ya hakimiliki za vitabu kati ya China na nchi zinazoshiriki kwenye mpango huo imeongezeka kwa kasi ya wastani ya asilimia 20 kwa mwaka. Bw. Liu Yehua ni mkurugenzi wa kituo cha uchapishaji wa kimataifa cha shirika la uchapishaji la Chuo Kikuu cha Umma cha China, anasema, "Shirika letu linauza aina zaidi ya 200 za vitabu vya lugha zaidi ya 20 katika nchi za nje kila mwaka. Kati ya vitabu hivyo, karibu asilimia 65 vinauzwa katika nchi zinazohusika na Ukanda moja, Njia moja."

  Yin Muyun ni mhariri mkuu wa Shirika la Uchapishaji la Chuo Kikuu cha Walimu cha mkoa wa Guangxi. Anaona wageni wameanza kufuatilia maisha ya wachina wa kawaida. Anasema, "Kwa mfano kitabu cha Pingru na Meitang, hadithi za sisi wawili kimeangizwa na nchi 7 za kigeni. Kwenye kitabu hiki, mwandishi alieleza hadithi mbalimbali kuhusu yeye na mke wake kupitia michoro na maandishi. Hadithi hizo zinaonesha mabadiliko ya maisha ya wachina katika miongo kadhaa iliyopita."

  Idara kuu ya habari, uchapishaji, radio na televisheni ya China hivi karibuni ilitoa ripoti kuhusu shughuli za habari na uchapishaji za mwaka 2016 nchini China. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana China iliagiza aina 16,587 za haki ya uchapishaji wa vitabu kutoka nchi za nje, na kuuza aina 8,328 katika nchi za nje. Habari zinasema vitabu vya nchi za nje vinavyopendwa zaidi na wachina, ni kuhusu utamaduni, sayansi za kijamii na vya kuelimisha watoto. Iran ni mgeni rasmi wa maonesho ya mwaka huu. Mashirika kadhaa kutoka nchi hiyo yameleta aina zaidi ya elfu moja za vitabu, haswa vitabu vya kuelimisha watoto. Bi Saideh Argani kutoka Iran anasema, "Tumeuza haki za kuchapisha vitabu kadhaa kwa mashirika ya China. Mwaka jana tulifikia makubaliano na Shirika la Uchapishaji la Yilin la China, na kuliidhinisha kuchapisha kitabu kimoja cha Iran. Mwaka huu kazi yetu muhimu ni kupata vitabu vizuri vya China. Zamani tulinunua vitabu vingi vya nchi za magharibi, na sasa tunataka vitabu bora vya nchi za mashariki. Tunatumai tutafikia makubaliano mengi zaidi na mashirika ya China katika maonesho hayo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako