• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimizwa kuharakisha hatua za kudhibiti matumizi sigara

    (GMT+08:00) 2017-08-24 19:13:13

    Mashirika 37 ya China yakiwemo kituo cha utafiti wa afya kwa majaribio mapya, shirikisho la udhibiti wa sigara la China na tawi lake mjini Beijing, hivi karibuni yametoa ripoti yakitangaza maoni manne ya pamoja na changamoto tisa zinazokabili juhudi za kudhibiti sigara. Wataalamu wamefahamisha kuwa, matumizi ya tumbaku nchini China yanachukua asilimia 44 ya matumizi hayo kote duniani, na kila mwaka wachina wanaofariki dunia kutokana na matumizi ya tumbaku wanazidi milioni moja. Wataalamu wanaitaka China iharakishe mchakato wa kutekeleza ahadi yake ya kudhibiti sigara, ili kutimiza lengo lake la kupunguza kiwango cha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 15 wanaovuta sigara kuwa chini ya asilimia 20 hadi kufikia mwaka 2030.

    Ikiwa nchi inayozalisha na kutumia tumbaku nyingi zaidi duniani, China ina watumiaji zaidi ya milioni 300 wa tumbabu, na zaidi ya nusu ya wanaume wazima wanavuta sigara. Utafiti umethibitisha kuwa, uvutaji sigara unaleta maradhi mengi yakiwemo ya mishipa ya moyo na ubongo na saratani, na ni sababu ya pili kwa binadamu kufariki baada ya ugonjwa wa shinikizo la damu.

    Mwaka 2003, China ilisaini mkataba wa mwongozo wa udhibiti wa tumbaku uliotungwa na Shirika la Afya duniani, ambao ulianza kutekelezwa rasmi nchini China kuanzia mwaka 2006. Kwa mujibu wa mwongozo wa mpango wa afya ya China wa mwaka 2030, hadi kufikia mwaka huo, kiwango cha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 16 wanaovuta sigara kitakuwa chini ya asilimia 20. Naibu mkuu wa shirikisho la udhibiti wa kuvuta sigara la China Bw. Zhi Xiuyi amesema, ili kutimiza lengo hilo, China inapaswa kuharakisha mchakato wa kutekeleza mkataba wa WHO.

    "Ingawa tumepiga hatua muhimu, lakini ikilinganishwa na matakwa ya mkataba wa WHO na mwongozo wa mpango wa afya ya China wa mwaka 2030, bado haitoshi. Kama hatutaharakisha mchakato wa kudhibiti sigara, China itaendelea kukumbwa na hasara kubwa kiafya, kiuchumi na kijamii."

    China ina sheria ya kupiga marufuku mashirika ya tumbaku kutoa matangazo, lakini baadhi ya mashirika hayaifuati kwa makini sheria hiyo. Bw. Zhi Xiuyi amezitaka idara zinazohusika za serikali ziimarishe nguvu ya kutekeleza sheria, na kuhamasisha umma kujiunga na kazi hiyo. Ripoti ya mwaka 2015 ya uchunguzi wa matumizi ya tumbaku ya watu wazima nchini China inaonesha kuwa, kiwango cha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 15 wanaovuta sigara nchini China ni asilimia 27.7, sawa na kiwango hicho cha mwaka 2010, lakini idadi ya watu wanaovuta sigara imeongezeka kwa watu milioni 15, na kufikia milioni 315. Watalaamu wanaona hatua ya kukabiliana na changamoto hii ni kuwaelimisha watoto na vijana, waepuke matumizi ya tumbaku. Naibu mkurungezi wa kituo cha utafiti wa maendeleo ya afya kwa majaribio mapya Bi. Wu Yiqun anasema,

    "Naona kazi yetu muhimu ni kupunguza watumiaji wapya wa tumbaku. Nakubali sana kufanya matangazo ya kudhibiti sigara katika shule na vyuo. Kwani hadi kufikia mwaka 2030, watoto wanaosoma a shule na vyuo watakuwa watu wazima. Tunapaswa kufanya juhudi zoteili wasivute sigara."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako