• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wakimbizi wanaokwenda Ulaya inapungua, lakini ukatili na vifo vinaendelea

    (GMT+08:00) 2017-08-25 09:22:15

    Idadi ya wakimbizi na wahamiaji waliofika Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imepungua, lakini wengi wa wanaokwenda Ulaya wanachagua kutumia wasafirishaji na mitandao ya hatari, na kuwa kwenye hatari ya vifo au ukatili mkali.

    Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR inasema idadi ya watu wanaovuka bahari ya Mediterranean kwa mwaka huu imepungua kwa kasi ikilinganishwa na mwaka jana, hasa kwa asilimia 94 ya watu wanaotumia njia ya bahari kutoka Uturuki kuingia Ugiriki.

    Hata hivyo licha ya idadi hiyo kupungua, uwezekano wa kufa kwa watu wanaojaribu kwenda Ulaya ni mkubwa sana, Katika kipindi hicho watu 2,253 walikufa au kupotelea baharini, na wengine 40 walikufa kwenye njia za ardhini au karibu na mipaka ya Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako