Ripoti ya maendeleo ya shughuli za roboti nchini China ya mwaka huu inaonyesha kuwa soko la roboti nchini China linapata maendeleo ya kasi, na China imekuwa soko kubwa zaidi duniani la roboti zinazotumiwa viwandani kwa miaka mitano mfululizo.
Mkurugenzi wa kituo cha utafiti na ushauri cha shirika la elektroniki la China Bw. Li Ting amesema mauzo ya roboti zinazotumiwa viwandani nchini China yanachukua theluthi moja hivi ya mauzo kwenye soko la dunia. Inakadiriwa kuwa mwaka huu idadi ya roboti zitakazouzwa nchini China itazidi 110,000, thamani ya mauzo itafikia dola za kimarekani bilioni 4.22, na thamani hiyo inatazamiwa kufikia dola za kimarekani bilioni 5.89 ifikapo mwaka 2020.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |