Mikataba ya miradi 10 imesainiwa kwenye mkutano wa mwaka 2017 wa baraza la madini kati ya China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN unaofanyika huko Nanning, ambayo thamani yake imefikia dola za kimarekani milioni 793.
Miradi 17 ilitangazwa kwenye mkutano huo, ikiwemo miradi katika mikoa ya Guangxi, Guangdong, Guizhou, na Gansu nchini China na katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia.
Kwenye mkutano huo shirika la madini la China limesaini waraka wa ushirikiano na shirika la madini la ASEAN.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |