• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kimataifa wa roboti wafungwa hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-08-28 17:48:07

    Mkutano wa kimataifa wa roboti umefungwa hapa Beijing. Tangu mkutano wa kimataifa wa roboti ufanyike kwa mara ya kwanza mwaka 2015, mkutano huo umehimiza mawasiliano na ushirikiano wa teknolojia ya roboti kote duniani, na umekuwa kama michezo ya Olimpiki ya shughuli ya roboti duniani. Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "Uvumbuzi, Kujiajiri, Kubuni na Kupokea Jamii ya Kisasa". Viongozi 300 hivi wa shughuli ya roboti kutoka China, Marekani, Russia, Uingereza na Ujerumani wamehudhuria mkutano huo, huku roboti za aina zaidi ya elfu moja zimeoneshwa na mashirika 150 hivi ya roboti ya ndani na nchi za nje kwenye mkutano huo. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong ametoa hotuba akisisitiza kuwa China itazidisha kutekeleza mkakati wa uvumbuzi kuhimiza maendeleo, kuunganisha mkakati wa "Made in China 2025" pamoja na "Internet Plus" ili kuharakisha maendeleo ya shughuli za roboti.

    Shirika la roboti la China HRG ni shirika lililofanya onesho kubwa zaidi katika mkutano huo kwa kuonesha roboti zaidi ya 50. Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, ambaye ni ofisa mkuu wa teknolojia Bw. Bai Xianglin amesema, kushiriki mkutano wa kimataifa wa roboti kuna maana kubwa kwa maendeleo ya shirika hilo.

    "Kupitia mkutano huo, tumetangaza chapa yetu, mkutano wa kimataifa wa roboti ni mkutano pekee tunaoshiriki nchini. Tumewafahamu wadau wengine wa shughuli ya roboti na kupata habari mpya za teknolojia ambazo zitatusaidia kupanga mpango na mkakati katika siku za baadaye. Mbali na hayo, tumetekeleza majukumu yetu kwenye mkutano huo. Tumewafahamisha wazee na watoto wengi waliokuja jinsi roboti zinavyofanya kazi, na matatizo yanayoweza kutatuliwa na roboti, Tumepata mafanikio mengi kwenye mkutano huo."

    Bw. Bai anatambua kuwa katika ubunifu wa roboti, China bado iko nyuma kuliko nchi nyingine zilizoendelea. Lakini ikilinganishwa na nchi zinazoongoza kwenye shughuli ya roboti, China ina nguvu bora katika jukwaa la utengenezaji wa roboti kwa kuwa na aina nyingi za bidhaa. Sera ya "Made in China 2025" imeweka bayana kuwa roboti zitakuwa kipaumbele cha maendeleo, na serikali itaunga mkono kupunguza pengo kati ya China na nchi zilizoendelea. Amesema,

    "Kwa upande wa teknolojia, pengo kati ya roboti za viwandani za China na nchi za nje bado ni kubwa. Lakini pengo hilo halitazibwa ndani ya muda mfupi. Aina za roboti zinazooneshwa na mashirika ya nchi za nje ni chache, lakini mashirika ya China yameonesha roboti za aina mbalimbali ambazo zinahusiana na sekta mbalimbali. Hii ni sifa ya kipekee ya roboti zinazotengenezwa na mashirika ya China. Jukwaa la mashirika ya China limeshirikisha watu hodari wenye ujuzi na teknolojia za juu. Nina imani kuwa katika siku za mbele tutapata maendeleo makubwa zaidi katika roboti zinazotoa huduma na za viwandani, na kupunguza pengo kati ya China na nchi zilizoendelea katika shughuli ya roboti. "

    Bw. Bai anaona kuwa katika siku za baadaye mahitaji ya roboti zinazotoa huduma katika soko la ndani yataongezeka.

    "Katika siku za baadaye, tutaendelea kujiendeleza katika utengenezaji wa roboti zinazotoa huduma, Mwelekeo wa maendeleo ya roboti za viwandani katika miaka mitano hadi kumi ijayo utakuwa katika kuendeleza ushirikiano kati ya binadamu na roboti. Tumekubaliana kuwa roboti za viwandani zitaendelezwa kuwa roboti za kisasa. Hivi karibuni, mahitaji ya roboti zinazotoa huduma yanaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa, kwa sababu roboti za aina hiyo zitahudumia kila familia na kila mtu. Soko la roboti zinazotoa huduma ni kubwa zaidi kuliko soko la roboti za viwandani. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako