• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za Ulaya na Afrika wafikia maoni ya pamoja kuhusu suala la wahamiaji haramu

    (GMT+08:00) 2017-08-29 16:38:42

    Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Italia, Libya, Niger na Chad na maofisa wa Umoja wa Ulaya wanaoshughulikia sera za diplomasia na usalama wamekutana mjini Paris na kutoa taarifa ya pamoja wakisema wamefikia maoni mengi ya pamoja kuhusu suala la wahamiaji haramu.

    Taarifa hiyo inasema nchi hizi zimekubali kuanzisha utaratibu mpya wa kuwahimiza na kuwasaidia wahamiaji haramu waliokwenda Ulaya kurudi nyumbani kwa hiari. Nchi hizo pia zimetoa wito kuyataka mashirika yote yasiyo ya kiserikali yanayofanya uokoaji katika bahari husika kusaini makubaliano ya kanuni za uokoaji baharini yaliyotungwa na Italia, ili kuboresha ufanisi wa uokoaji na kuimarisha uratibu kati ya makundi mbalimbali ya uokoaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako