• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Meli ya hospitali ya jeshi la China yafanya operesheni ya kutoa huduma barani Afrika

  (GMT+08:00) 2017-08-29 18:20:41

  Meli ya hospitali ya Peace Ark ya jeshi la majini la China inayofanya operesheni ya "majukumu ya masikilizano ya 2017" imewasili Djibouti, na kutoa huduma bure za tiba kwa wakazi zaidi ya elfu moja wa huko. Hii ni mara ya sita kwa meli hiyo kufanya ziara kama hiyo. Kamanda wa operesheni hiyo Guan Bolin amesema, meli ya Peace Ark inatangaza ubinadamu, upendo na moyo wa kujitolea, na pia imesambaza wazo la maendeleo na ushirikiano wa amani la China na kuonesha taswira ya nchi kubwa inayotekeleza majukumu yake na moyo wa kujiamini na kuwa wazi kwa jeshi la majini la China. Fadhili Mpunji anatuandalia ripoti ifuatayo.

  Meli ya hospitali ya Peace Ark ilifunga safari kutoka bandari ya kijeshi ya Zhoushan Julai 26 na kuanza kutekeleza operesheni ya "majukumu ya masikilizano ya 2017", na kufanya ziara nchini Djibouti, Sierra Leone, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Angola, Msumbiji, Tanzania na Timor Mashariki na kutoa huduma ya matibabu kwa muda unaokadiriwa siku 155. Hii ni mara ya sita kwa meli hiyo kufanya operesheni ya kutoa huduma ya matibabu tangu mwaka 2010. Kamanda wa operesheni meja jenerali Guan Bolin alipozungumzia maana ya operesheni hiyo, amesema,

  "Operesheni ya Majukumu ya Masikilizano ya 2017 imepitishwa na kamati kuu ya jeshi la China, na kuorodheshwa katika shughuli muhimu za kidiplomasia na kijeshi katika mpango wa mwaka. Operesheni hiyo ni sehemu ya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa na China, na pia ni jukumu muhimu la huduma za matibabu kwa jeshi la majini la China kusafari mbali, na imezidisha na kupanua mfululizo wa operesheni ya majukumu ya masikilizano."

  Guan Bolin ameshiriki kwenye operesheni hiyo mara ya nne, na hii ni mara yake ya pili kushika wadhifa wa kamanda, anasema,

  "Meli ya Peace Ark inatangaza ubinadamu, upendo na moyo wa kujitolea, kueneza wazo la maendeleo na ushirikiano wa amani la China, huku ikionesha taswira ya nchi kubwa inayotekeleza majukumu na moyo wa kujiamini na kuwa wazi kwa jeshi la majini la China. Kwa upande wa siasa na mkakati, operesheni hiyo ina umuhimu mkubwa katika ushirikiano kati ya China na nchi zinazotembelewa."

  Kamanda huyo amesema, katika operesheni hiyo, meli hiyo itatoa huduma za matibabu kwa wanajeshi wa msafara wa manowari ya jeshi la majini la China, askari na wafanyakazi katika kituo cha uungaji mkono nchini Djibouti, huku ikitoa huduma bure kwa wafanyakazi wa ubalozi wa China, wachina wanaoishi huko na wanafunzi wanaosoma huko. Amesema,

  "Meli hiyo itatoa huduma mbalimbali za matibabu, mbali na wagonjwa kupatiwa matibabu kwenye meli, tuna kikosi cha kukinga maradhi ambacho kinaweza kutatua masuala ya kuondoa, kuangamiza na kutokomeza maradhi ya huko, na kuwafahamisha wakazi wa huko ujuzi husika wa afya. Aidha, tutatuma kikundi cha wataalamu kufanya mawasiliano na ushirikiano katika hospitali za huko na kutoa mafunzo kwa madaktari wa huko. "

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako