China imefanikiwa kuwaondoa watu milioni 13.91 kwenye umasikini kila mwaka kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka jana, na kipato cha mwaka kwa maeneo masikini zaidi kimeongezeka na kufikia asilimia 10.7 kila mwaka.
Hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa na Baraza la Serikali la China kuhusu kazi ya kupunguza umasikini iliyowasilishwa kwenye kikao cha siku tano cha Kamati Kuu ya Bunge la Umma la China kilichoanza jana.
Mkurugenzi wa ofisi ya kupambana na umaskini ya baraza la serikali ya China Bw. Liu Yongfu amesema, baraza hilo limeweka juhudi kubwa katika kuondoa umasikini, na kwamba ripoti ya kazi za serikali kwa miaka minne iliyopita iliahidi kuondoa watu milioni 10 kutoka kwenye uamsikini.
China imeweka lengo la mwaka 2020 kuwa mwaka wa mwisho wa kujenga jamii yenye ustawi wa kati, lengo linalohitaji kuondolewa kwa umasikini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |