• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaimarisha usalama kwenye mpaka wake na Sudan Kusini baada ya mapambano ya wikiendi

    (GMT+08:00) 2017-08-30 09:26:02

    Jeshi la Uganda limeimarisha usalama kwenye mpaka wake na Sudan Kusini baada ya mapambano yaliyotokea wikiendi kusababisha vifo vya watu 19, akiwemo raia mmoja wa Marekani.

    Akieleza kuhusu hatua hiyo msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire, amesema usalama umeimarishwa kwenye mpaka wa Kaya, ili kuhakikisha pande zinazopambana za Sudan Kusini hazivuki mpaka na kuingia Uganda bila kujulikana. Amesema wataendelea kuwachunguza watu wote wanaotoka Sudan Kusini na kukikimbilia Uganda.

    Hata hivyo Bw Karemire amesema jeshi litaendelea kuwaruhusu wakimbizi kuingia Uganda.

    Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, zaidi ya wakimbizi milioni moja kutoka Sudan Kusini wameingia Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako