• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Kampuni za China kuwekeza katika sekta ya mafuta Uganda

    (GMT+08:00) 2017-08-30 20:02:33

    Kampuni za China zimeonyesha nia ya kushirikiana na bisahara za Uganda na kushiriki katika kuendeleza sekta za mafuta na gessi nchini Uganda.

    Akizungumza katika kongamano la mafuta na gesi jijini Kampala lililoandaliwa na Benki ya Stanbic Uganda kwa ushirikiano na Benki ya Biashara na Viwanda ya China (ICBC),Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Stanbic Patrick Mweheire,amesema hivi sasa kuna fursa nyingi sana katika sekta ya mafuta na gesi.

    Alisema shughuli nyingi zinaendelea,zabuni nyingi zinatolewa,na matarajio ni kwamba uamuzi wa mwisho wa uwekezaji kwa ajili ya mradi huu utatolewa katika robo ya kwanza ya mwaka ujao.

    Sekta ya mafuta na gesi inatarajiwa kuvutia uwekezaji wa takriban $15 bilioni (Shs54 trillion) huku kiasi kikubwa cha mtaji kikielekezwa katika ujenzi wa miundombinu.

    Mweheire amesema upatikanaji wa kiwango kikubwa cha mafuta na gesi nchini Uganda umevutia wengi na huenda ukaleta mageuzi katika uchumi wa nchi hiyo.

    Meneja wa kampuni ya uchimbaji mafuta ya Tullow nchini Uganda Jimmy Mugerwa amesema uwekezaji unaotarajiwa huenda ukaongeza mara mbili pato la taifa,na hatimaye kuongea pato la kila mwananchi.

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mafuta Uganda (PAU) Ernest Rubondo, alisema serikali itahakikisha kwamba kampuni za Uganda zinashiriki kikamilifua katika sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako