Mkutano wa Baraza la serikali la China uliofanyika jana umeamua kuchukua hatua kuboresha mazingira kwa ajili ya uvumbuzi na maendeleo. Uamuzi huo ulitolewa kufuatia kupatikana maendeleo kwenye mageuzi ya mwanzo katika kuboresha mazingira ya kitaasisi na kwenye soko kwa ajili ya ujasiriamali na uvumbuzi. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema, serikali itaunga mkono zaidi makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati, na kuimarisha hatua za kulinda hakimiliki za uvumbuzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |