• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yaipongeza Kenya kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki

    (GMT+08:00) 2017-08-31 09:00:53

    Shirika la maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD limeipongeza Kenya na Wizara yake ya Mazingira na Maliasili kwa kuchukua hatua ya kishujaa katika kupiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, marufuku hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mazingira ya kiafya ya binadamu na wanyama, na pia ukuaji wa uchumi wa kanda hiyo.

    Wakati huohuo, serikali ya Kenya imerejea tena ahadi yake ya kufanya majadiliano na wazalishaji ili kumaliza mvutano kuhusu marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira nchini Kenya Geoffrey Mahungu amesema, majadiliano hayo yatafanyika hivi karibuni ili kupata suluhisho mwafaka kutokana na mgogoro unaohusika na marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki iliyoanza kutekelezwa jumatatu wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako