• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kuzindua chanjo ya polio kwa watoto

    (GMT+08:00) 2017-08-31 09:52:12

    Wizara ya afya ya Uganda imetangaza kampeni ya kutoa chanjo ya polio mlango kwa mlango, ili kuzuia kuingizwa tena kwa virusi vya polio kutoka nchi jirani.

    Msemaji wa wizara hiyo Bibi Vivian Nakalika Sserwanja amesema, kampeni hiyo ya siku tatu itakayozinduliwa Septemba 9 inawalenga watoto milioni 5.7 walio na umri wa chini ya miaka mitano katika sehemu 73 zenye hatari zaidi, hasa watoto walio katika mpaka na Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Amesema, timu ya wahudumu wa afya wanaotoa chanjo hiyo wataenda nyumba kwa nyumba, kwenye masoko, mitaani na sehemu mbalimbali ili kuwapatia watoto chanjo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako