• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza muda tume ya AU nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-08-31 10:14:47

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilipitisha uamuzi wa kuongeza muda Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM hadi Mei 31 mwaka ujao na kupunguza idadi ya askari.

    Baraza hilo limeamua kupunguza idadi ya askari kutoka 22,126 wa sasa hadi 21,626 mwishoni mwa mwaka huu, na kufikia 20,626 ifikapo Oktoba 30 mwaka ujao.

    Uamuzi huo mpya umesema, lengo la muda mrefu kwa Somalia ni kuwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo vitakabidhiwa majukumu yote ya kulinda usalama nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako