• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China imetoa huduma ya kibiashara mara 55 kurusha satilaiti kwa ajili ya nchi nyingine

  (GMT+08:00) 2017-08-31 16:35:04

  Kampuni ya sayansi na teknolojia ya anga ya juu ya China CASC imetoa huduma ya kibiashara mara 55 kurusha satilaiti kwa ajili ya nchi nyingine, na itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwenye eneo hilo.

  Kwenye mkutano wa 3 wa baraza la ngazi ya juu la safari za anga ya juu za kibiashara la China, meneja mkuu anayeshughulikia masoko ya kikanda wa kampuni hiyo Bw. Si Yuan, amesema kampuni hiyo inashiriki kwenye ushindani wa kimataifa kwa mauzo ya satilaiti na huduma ya kurusha satilaiti. Tokea karne hii ianze, kampuni hiyo imetoa huduma za kurusha satilaiti kwa nchi mbalimbali zikiwemo Nigeria, Pakistan, Belarus na Laos, na baadhi ya nchi zenye nia ya kufanya safari za anga ya juu zinaendelea kutengeneza satilaiti zitakazorushwa na kampuni hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako