• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya jumla ya magari yanayotumia nishati mpya nchini China yazidi milioni 1

    (GMT+08:00) 2017-08-31 18:30:24

    Naibu mkuu wa shirika la viwanda vya magari la China Bw. Dong Yang amesema, katika miaka miwili iliyopita, utengenezaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme umepata maendeleo ya kasi, hadi sasa mauzo ya jumla ya magari yanayotumia nishati mpya nchini China yamezidi milioni 1, ambalo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 200 kwa mwaka. Idadi ya magari ya nishati mpya yaliyouzwa na yaliyotumiwa nchini China kwa mwaka jana, ilikuwa zaidi ya asilimia 50 ya idadi ya dunia.

    Bw. Dong amesema hivi sasa China kimsingi imeanzisha mfumo wa viwanda vya magari ya nishati mpya, ambao ni pamoja na viwanda vinayozalisha betri, injini na magari, na ujenzi wa mtandao wa kuchaji betri ya magari hayo pia unaendelea vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako