• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Ethiopia yakusanya dola milioni 460 za kuendeleza ujenzi wa bwawa

    (GMT+08:00) 2017-08-31 19:17:45

    Ethiopia imekusanya dola milioni 460 kutoka kwa uuma za kuendeleza ujenzi wa bwawa kubwa zaidi la kuzalisha kawi barani Afrika katika mto wa Blue Nile.

    Bwawa hilo lililoko kilomita 40 kutoka mpaka wa Ethiopia na Sudan linatarajiwa kuzalisha megawati 6,450 za kawi

    Mkuu wa mawasiliano kwenye baraza la kitaifa la kuratibu ushirikishi wa uuma bwana Hailu Abraham, amesema hata hivyo wanahitaji hado dola nilioni 560 kwa mradi huo.

    Ujenzi wa bwawa hilo ulianza mwaka 2011 na linatarajiwa kugharimu dola bilioni 4.7.

    Amesema sasa ujenzi umefikia asilimia 60 na serikali inatarajia kuweka mitambo miwili ya kuzalisha megawati 375 kwa majaribio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako