• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yaamuru kufungwa kwa ofisi ya Ubalozi wa Russia mjini San Francisco

    (GMT+08:00) 2017-09-01 08:48:19

    Marekani imeitaka Russia kufunga ofisi yake ya ubalozi mjini San Francisco, na kupunguza shughuli zake za kibalozi katika ofisi zake za ubalozi mjini Washington na New York kabla ya kesho. Hatua hii imekuja wiki chache baada ya Rais Vladmir Putin wa Russia kuiamuru Marekani ipunguze wanadiplomasia wake nchini Russia.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bibi Heather Nauret amesema Marekani imetekeleza kikamilifu uamuzi wa serikali ya Russia kupunguza wanadiplomasia wake, na kuona kuwa uamuzi wa Russia haukuhitajika na unaathiri uhusiano.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya ubalozi wa Russia mjini San Francisco inasema uamuzi wa Marekani ni hatua nyingine ya serikali ya Marekani itakayowaathiri warussia wanaoishi kwenye maeneo ya ofisi hiyo, pamoja na wamarekani. Mwaka jana ofisi hiyo ilitoa visa elfu 16 za utalii kwa wamarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako