• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UNDP asema nchi za BRICS zatoa ishara nzuri

    (GMT+08:00) 2017-09-01 08:55:16

    Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bw. Achim Steiner amesema, nchi za BRICS zinatoa ishara nzuri kwa dunia katika amani na maendeleo.

    Bw. Steiner amesema anatumai kupitia mkutano wa kilele wa nchi za BRICS utakaofanyika wiki ijayo huko Xiamen, China, nchi hizo zinazojitokeza kiuchumi zinaweza kutoa mchango katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili binadamu.

    Amesema mageuzi ya kiuchumi katika miaka zaidi ya kumi iliyopita sio tu yameziinua nchi hizo kiuchumi, bali pia yametoa jukwaa la kushawishi maendeleo ya dunia.

    Pia amesema, nchi hizo sio tu zinaangalia maslahi yao, bali pia zinazingitia maslahi ya pamoja, ambayo ni wazo kuu la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako