• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya tatu ya mazungumzo ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya haijapata matokeo mazuri

    (GMT+08:00) 2017-09-01 18:16:14

    Duru ya tatu ya mazungumzo ya siku nne kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo haikupata mafanikio kutokana na tofauti kubwa kati ya pande hizo mbili, hivyo kuongeza wasiwasi kwa wafanyabiashara wa Uingereza.

    Mkuu wa jumuiya ya biashara ya Uingereza Adam Marshall amesema, pande hizo mbili zinapaswa kutoa kipaumbele kwa kazi za muda wa mpito hasa katika utaratibu wa forodha ili kuongeza imani kwa makampuni ya pande hizo mbili.

    Habari zinasema, Umoja wa Ulaya unashikilia kujadili kwanza masuala ya fedha za kujitoa, haki za raia wa Umoja huo na mpaka wa Ireland Kaskazini. Lakini Uingereza inatarajia kutatua uhusiano wa kibiashara kati yao na mpango wa muda wa mpito.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako