• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Moscow kujibu vikali hatua za uhasama za Marekani

  (GMT+08:00) 2017-09-01 19:18:05

  Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov amesema nchi hiyo itajibu vikali hatua za kiuhasama za Marekani zinazoilenga Russia, ambazo zimetolewa kwa lengo la kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Lavrov alikuwa akizungumzia hatua ya Marekani ya kufunga ubalozi mdogo wa Russia huko San Fransisco, na ofisi nyingine mbili za ziada za kibalozi mjini Washington na New York ifikapo kesho. Hatua hiyo ya Marekani imetokana na uamuzi wa Russia wa kupunguza wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani nchini humo kuendana na idadi ya wanadiplomasia wa Russia nchini Marekani.

  Hata hivyo, Lavrov hakufafanua hatua itakayochukuliwa na Russia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako