• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha uchunguzi wa sayari ya Venus cha Japan chagundua upepo mkali kwenye ikweta ya sayari hiyo

    (GMT+08:00) 2017-09-01 20:07:25

    Data zilizokusanywa na chombo cha uchunguzi wa sayari ya Venus cha Japan zinaonesha kuwa kuna upepo mkali karibu na ikweta ya sayari hiyo, ambao una mwendo kasi zaidi ya mita 80 kwa sekunde. Ugunduzi huo huenda ukasaidia kufichua siri ya mzunguko mkubwa wa hewa kwenye sayari hiyo.

    Watafiti wa Japan wamesema ingawa hawawezi kupima mwendo kasi wa upepo moja kwa moja, lakini kuna mawingu mazito kwenye anga yenye urefu wa kilomita 45 hadi 70 kutoka ardhini, na wanaweza kukadiria mwendo kasi wa upepo kwa mujibu wa umbo wa mawingu. Inakadiriwa kuwa mwendo huo katika eneo lililoko karibu na Ikweta huwa ni kati ya mita 50 kwa sekunde hadi mita 70 kwa sekunde.

    Lakini baada ya kuchambua data zilizotumwa na chombo cha uchunguzi wa sayari hiyo mwezi Julai na Agosti mwaka jana, na kugundua kuwepo kwa upepo mkali wenye mwendo kasi zaidi ya mita 80 kwa sekunde. Kabla ya hapo wanajimu hawajawahi kuona upepo huo.

    Sayari ya Venus ina ukubwa unaofanana na dunia, lakini tabaka la hewa kwenye sayari hiyo likiathiriwa na upepo kutoka magharibi linakuwa kwenye hali ya mzunguko mkubwa, hata mwendo kasi wa hewa unakuwa kwa makumi ya mwendo kasi wa mzunguko wa sayari hiyo. Wanasayansi bado hawajajua sababu ya hali hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako