• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za BRICS zatakiwa kuenzi mawazo sahihi kuhusu usalama

    (GMT+08:00) 2017-09-03 16:37:47

    Nchi za BRICS zimetakiwa kuenzi mawazo endelevu ya pamoja na ya jumla ambayo yanazingatia ushirikiano kuhusu hali ya usalama, kujiunga na kuchangia utatuzi wa masuala muhimu ya kikanda kwa msimamo wa kiujenzi. Rais Xi Jinping wa China amesema hayo alipohutubia ufunguzi wa kongamano wa viwanda na biashara kati ya nchi za BRICS. Ametoa ufafanuzi kwamba, nchi hizo ni walinzi wa amani ya dunia, na wajenzi wa utaratibu wa usalama wa kimataifa. Hivyo zinatakiwa kulinda kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa, sheria ya kimsingi kuhusu uhusiano wa kimataifa, na ushirikiano kati ya nchi nyingi katika utatuzi wa masuala ya kikanda na kimataifa, na kuhimiza uhusiano wa kimataifa uwe wa kidemokrasia, kupinga vitendo vya umwamba na siasa kali katika mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako