• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chansela wa Ujerumani atetea sera ya wakimbizi huku akishambuliwa na mpinzani wake kwenye mdahalo wa TV

    (GMT+08:00) 2017-09-04 09:23:34

    Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amesema licha ya kuwa waislamu wenye siasa kali wanaochochea matendo ya kigaidi barani Ulaya, bado anaamini kuwa "uislamu ni wa Ujerumani".

    Bibi Merkel ametoa kauli hiyo kwenye mdahalo uliorushwa kwa njia ya Televisheni na mpinzani wake mkubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao Bw Martin Schulz, wakati suala la wakimbizi na wahamiaji likiwa ni suala linalofuatiliwa zaidi kwenye mdahalo huo.

    Wagombea wote wamesema hakuna tatizo na wahamiaji waislamu, lakini Bibi Merkel amesema msukosuko wa wakimbizi wa mwaka 2015 umeiachia Ujerumani jukumu gumu la kuwajumuisha watu hao kwenye jamii, na kutakiwa kuhakikisha wanapatiwa elimu na kazi.

    Bw Shultz amemkosoa Bibi Merkel kwa kutokuwa na msimamo mmoja na wenzake wa Ulaya kwenye suala la wakimbizi mwanzoni mwa mwaka 2015. Bibi Merkel ametetea uamuzi wake na kusema lazima kuwa na ukaguzi mkali zaidi kwa watu wanaotaka kuhamia Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako