• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu watoa maelezo kuhusu hotuba ya rais Xi Jinping katika kongamano la viwanda na biashara la BRICS

    (GMT+08:00) 2017-09-04 09:44:29

    Rais Xi Jinping wa China alihudhuria na kuhutubia Ufunguzi wa Kongamano la viwanda na biashara kati ya nchi za BRICS lililofunguliwa mjini Xiamen, China. Wataalamu wanaona hotuba hiyo ya rais Xi imeweka msingi wa maendeleo ya nchi za BRICS katika miaka 10 ijayo, na mfumo wa ushirikiano kati ya nchi hizo utazidi kukuzwa katika siku za baadaye.

    Hotuba ya rais Xi imejumuisha moyo wa BRICS: "kutendeana kwa usawa, kutafuta maslahi ya pamoja na kuheshimu tofauti miongoni mwao; kufanya ushirikiano wenye ufanisi na ushirikiano wa kunufaisha pande zote; na kuchukua mtizamo wa kuzisaidia nchi nyingine duniani kupata maendeleo. Mtafiti wa Taasisi ya uhusiano wa kimataifa wa kisasa wa China Bibi Chen Fengying akizungumzia hotuba hiyo anasema:

    "Kanuni ya kwanza iliyotajwa kwenye hotuba ya rais Xi ni kuwa nchi zote za BRICS ni sawa, na zinatendeana kwa usawa, hii vilevile ni kanuni muhimu zaidi ya kuziunganisha nchi za BRICS. Aidha, ingawa nchi hizo zinatoka mabara tofauti, zinatafuta maslahi ya pamoja wakati zinaheshimu uwepo wa tofauti kati yao. Pia zinafanya ushirikiano wenye ufanisi ambao utaleta mafanikio halisi. Pia zina lengo la kuzisaidia nchi nyingine zinazoibuka kiuchumi na nchi zinazoendelea duniani ili kuleta mabadiliko duniani."

    Mkurugenzi wa Kituo cha ushirikiano kuhusu nchi za BRICS katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing Bw. Wang Lei akizungumzia hotuba hiyo ya rais Xi, anasema:

    "Hotuba ya Rais Xi pia inatoa wito wa kuwa na imani kwa ushirikiano kati ya nchi za BRICS, kwa kuwa ushirikiano huo unafanyika kwa kutegemea soko kubwa na raslimani nyingi za nchi hizo tano. Hivi sasa nchi hizo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za ndani na kutoka nje ya mfumo wa BRICS, lakini hatua mbalimbali za mageuzi zilizotekelezwa katika miaka mingi iliyopita zitaleta matokeo mazuri na kuwa msukumo kwa ushirikiano kati ya nchi hizo katika siku za baadaye."

    Kwenye hotuba hiyo, rais Xi Jinping ametoa mapendekezo manne kuhusu maendeleo ya nchi za BRICS katika miaka 10 ijayo, yakiwa ni pamoja na : kuendeleza ushirikiano kati ya nchi za BRICS, kuhimiza msukumo wa ongezeko la uchumi wa nchi hizo; kubeba majukumu ya kulinda amani na usalama duniani; kuonesha umuhimu wa nchi za BRICS na kukamilisha ushughulikiaji wa mambo ya uchumi duniani; kuongeza ushawishi wa nchi hizo, na kupanua zaidi uhusiano wa kiwenzi kati yao. Bibi Chen Fengying akizungumzia mapendekezo hayo yaliyotolewa na rais Xi anasema:

    "Kati ya mapendekezo hayo, ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za BRICS unapewa kipaumbele. Pia rais Xi Jinping kwa mara ya kwanza alitoa wazo la kulinda usalama na amani ya dunia, kutokana na umuhimu wa ushirikiano wa usalama wa kisiasa. Jambo muhimu zaidi ni kuwa, rais Xi alisisitiza kuwa inapaswa kuonesha umuhimu wa nchi za BRICS, na kupanua zaidi ushawishi wa nchi hizo. Hotuba hiyo imeonesha mwelekeo wa maendeleo ya nchi hizo katika miaka 10 ijayo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako