• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini ina matarajio makubwa kwa mkutano wa kilele wa BRICS Xiamen

    (GMT+08:00) 2017-09-04 10:28:51

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema utaratibu wa mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS utasaidia nchi yake kukabiliana na suala la umaskini, ukosefu wa ajira na kutokuwa na uwiano wa mgawanyiko, na pia utachangia kutimiza malengo ya milenia kwa nchi zinazoendelea.

    Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti ya nchi za BRICS katika kamati ya utafiti ya sayansi na utamaduni ya Afrika Kusini Jaya Josie, amesema wanatarajia kuanzishwa kwa shirika la kutathmini uwezo wa nchi wa kulipa madeni la BRICS, ambalo litakuwa nyongeza kwa mfumo uliopo wa tathmini wa kimataifa.

    Mtafiti wa mradi wa uchumi na diplomasia wa taasisi ya utafiti ya mambo ya kimataifa ya Afrika Kusini, Cyril Princeloo anaona kuwa, nchi za BRICS zinatakiwa kufuatilia maendeleo endelevu, anatumai kuwa nchi za BRICS zitawekeza zaidi barani Afrika, kuisaidia Afrika kuongeza thamani ya bidhaa na kuboresha muundo wa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako