• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Siafu anatoa mbolea kwa mimea

  (GMT+08:00) 2017-09-04 15:27:06

  Wanasayansi wa Denmark wamegundua kuwa siafu wanaoishi kwenye mibuni wanatoa kinyesi kwenye miti hiyo, na kitendo hiki kisichojulikana na watu huenda kina umuhimu mkubwa kwa ukuaji wa mimea hata mazingira ya viumbe.

  Hali ya kunufaishana kati ya mimea na siafu inaonekana mara kwa mara, kwa mfano, baadhi ya mimea inatoa asali ili kuwavutia siafu, na siafu wanaisaidia kufukuza wadudu wanaoharibu mimea, kiota cha siafu kinasaidia kuboresha udongo na kutoa lishe kwa mimea. Lakini katika ukanda wa tropiki, siafu wengi wanaishi juu ya mimea badala ya ardhini, kama siafu hao wanatoa lishe kwa mimea au la bado haijulikani.

  Watafiti wa Chuo Kikuu cha Aarhus cha Denmark wamechunguza siafu aina ya Oecophylla Smaragdina kwenye nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea ili kutafiti athari ya siafu hao kwa mibuni. Siafu hao wanatapakaa katika ukanda wa tropiki na kanda zilizoko karibu, wanaishi juu ya miti, na ni siafu wakali ambao wana uwezo mkubwa wa kuwakamata wadudu wengine. Watafiti wametia asidi ya Amino yenye Nitrogen-15 kwenye chakula cha siafu na kuchunguza Nitrogen inakwenda wapi. Baadaye wakagundua kuwa kwenye majani ya miti inayofikiwa na siafu kuna Nitrogen nyingi zaidi, na miti inakua vizuri zaidi kuliko ile isiyofikiwa na siafu. Watafiti wamesema hali hii inaonesha kuwa siafu wanaweza kutoa mbolea kwa mimea, na ni muhimu kwa mazingira ya viumbe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako