• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi tano za BRICS zatangaza azimio la Xiamen

    (GMT+08:00) 2017-09-04 15:47:57
    Mkutano wa tisa wa viongozi wa nchi zinazounda kundi la BRICS umefunguliwa leo asubuhi mjini Xiamen, China. Rais Xi Jinping wa China ameendesha mkutano huo unaohudhuriwa na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, rais Michel Temer wa Brazil, rais Vladimir Putin wa Russia na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi. Mkutano huo umepitisha azimio la Xiamen, linaloelekeza kuwa hizo tano zitazidisha ushirikiano halisi katika sekta za uwekezaji wa biashara, fedha, uvumbuzi na nishati. Pia limetoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu kikanda na kimataifa, na kusisitiza kuwa nchi hizo zitafanya juhudi kwa pamoja ili kuzidisha uhusiano wa urafiki na kimkakati, na kuanzisha miaka 10 ya pili ya ushirikiano kati ya nchi hizo.Rais Xi Jinping amesema, kutokana na mabadiliko makubwa duniani, ushirikiano kati ya nchi za BRICS ni muhimu zaidi. Nchi hizo zinapaswa kuhimiza ushirikiano halisi wa uchumi, kuimarisha uungaji wa mkakati wa maendeleo, kuhimiza utaratibu wa kimataifa uelekee kuwa na usawa na haki zaidi, na kuimarisha mawasiliano ya utamaduni ya kijamii.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako