• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafunzo ya sheria ya kimataifa yanayohusisha wajumbe kutoka Afrika na Asia yafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-09-04 18:56:08

    Wataalam 50 wa sheria na maofisa kutoka nchi za Asia na Afrika, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Ushauri wa Kisheria ya Afrika na Asia (AALCO) wamekutana katika semina ya mafunzo kuhusu sheria ya kimataifa inayofanyika hapa Beijing, China.

    Semina hiyo imeandaliwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Wuhan na Kitivo cha Sheria ya Kimataifa cha Asia na itamalizika tarehe 24 mwezi huu.

    Waandaaji wa semina hiyo wamesema, wataalam 13 wa sheria ya kimataifa watatoa mihadhara katika semina hiyo, akiwemo rais wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa Shi Jiuyong na katibu mkuu wa AALCO Kennedy Gastrom.

    Semina hiyo itatoa mafunzo kadhaa kuhusu sheria ya kimataifa na kuimarisha mawasiliano kati ya nchi za Asia na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako