• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Colombia na upinzani zasaini makubaliano ya kusitisha vita

    (GMT+08:00) 2017-09-05 09:27:29

    Serikali ya Colombia na kundi la upinzani la ELN wamesaini makubaliano ya kusitisha vita kwa muda katika mji mkuu wa Ecuador, Quito, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kukomesha mapambano kati ya pande hizo mbili yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 50. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande hizo mbili zitasitisha mapambano kwa siku 102 kuanzia Oktoba mosi. Waziri wa mambo ya nje wa Ecuador Bi. María Fernanda Espinosa Garcés amepongeza kusainiwa kwa makubaliano hayo, na kusema yanamaanisha mchakato wa amani wa Colombia na kanda ya Latin Amerika utapiga hatua kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako