• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yakanusha madai ya waasi kuhusu juhudi za kikanda za kumuweka huru Riek Machar

    (GMT+08:00) 2017-09-05 09:40:42

    Sudan Kusini imekanusha madai ya waasi juu ya juhudi zinazoendelea za kumuweka huru aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar anayeishi uhamishoni nchini Afrika Kusini.

    Akikanusha madai hayo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini Mawien Makol amesema taarifa za karibuni zilizotolewa na waasi wa SPLA wa upinzani, zinazosema kwamba wajumbe muhimu wa nchi za Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Masharik IGAD wanafanya juhudi ili kumuondoa uhamishoni Machar, si sahihi. Makol amesema hivi sasa wapo kwenye makubaliano na wapinzani wa SPLA chini ya Taban Deng Gai aliyechukua nafasi ya Machar.

    Awali, naibu msemaji wa waasi Brigedia William Deng Gatjiath alisema Sudan, Kenya na Ethiopia zinaendelea na juhudi za kumuweka huru kiongozi wao kutoka uhamishoni.

    Machar alikimbia Juba baada ya mapambano mapya kati ya jeshi la serikali na waasi yaliyotokea Julai 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako