• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yalaani jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini

  (GMT+08:00) 2017-09-05 10:26:43

  Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amelaani jaribio jipya la nyuklia la Korea Kaskazini na kuitaka nchi hiyo irudi kwenye mazungumzo.

  Bw. Liu amesema, kitendo hicho kimekiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba China inatarajia kuwa Korea Kaskazini itazingatia msimamo wa jumuiya ya kimataifa wa kuondoa silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea na kuchukua hatua kuzuia hali ya eneo isiwe mbaya zaidi.

  Habari zinasema, rais Donald Trump wa Marekani amezungumza na wenzake wa Korea Kusini na Ujerumani kuhusu suala la nyuklia katika peninsula ya Korea. Ikulu ya Marekani imesema, rais Trump na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini wamekubaliana kutumia uwezo wao wote kuweka shinikizo zaidi kwa Korea Kaskazini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako