• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yaitaka Marekani iunge mkono mchakato wa amani nchini humo

    (GMT+08:00) 2017-09-05 10:27:02

    Sudan Kusini imeitaka Marekani kuunga mkono jitihada za nchi hiyo katika kulinda amani badala ya kuangalia upya sera kuhusu hali ya sasa ya nchi hiyo.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini Mawien Makol amesema hayo kufuatia kauli zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani USAID, Mark Green alipofanya ziara nchini humo, kuwa serikali ya rais Donald Trump inafikiria upya kumuunga mkono rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.

    Amesema serikali inadhamiria kuleta amani kupitia mjadala wa kitaifa, na inasaidia kufungua njia ya kupeleka misaada ya kibinadamu kwa kusaidiana na jeshi la SPLA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako