• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AIIB yatangaza kutoa dola milioni 210 kwa ajili ya mradi wa nishati endelevu kwa Misri

    (GMT+08:00) 2017-09-05 18:39:15

    Benki ya maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu ya Asia AIIB imetangaza kuipatia Misri dola milioni 210 kwa ajili ya miradi wa nishati endelevu.

    Taarifa iliyotolewa na benki hiyo imesema mradi huo utakuwa na vituo 11 vya nishati ya jua vitakavyokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 490.

    Makamu mkuu wa Benki hiyo Bw. Pandian amesema wamekubali kuchangia kwenye mradi huo, kwa kuwa utatoa mchango kwa Misri kuwa kituo cha uzalishaji wa nishati, na kuisaidia Misri kutekeleza majukumu yake kwenye mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mradi huo utafadhiliwa AIIB na benki ya dunia, na wakopeshaji wengine binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako