• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yateua watu sita kusimamia uchaguzi wa rais wa marudio

    (GMT+08:00) 2017-09-06 09:31:04

    Tume ya uchaguzi ya Kenya imeteua timu ya watu sita kusimamia uchaguzi wa rais wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Wafula Chebukati ametangaza kuwateua watu hao ambao amesema watafanya kazi kwa muda wa miezi mitatu. Ametangaza kumteua Bw Marijani Hussein Marijani kuwa mratibu wa uchaguzi, Bw Sidney Namulungu kuwa mkuu wa operesheni na Bw Albert Gogo kuwa mkuu wa Tehama.

    Mabadiliko hayo yamekuja wakati kiongozi wa muungano wa upinzani Bw Raila Odinga, ametishia kutoshiriki kwenye uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 17, kama hakutakuwa na uhakikisho wa kisheria na kikatiba. Ametaka kuwe na mabadiliko ya maofisa wa tume ya uchaguzi, na teknolojia ya ukaguzi wa matokeo iendane kikamilifu na sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako