• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xi Jinping apongeza ufunguzi wa maonesho ya China na nchi za kiarabu

  (GMT+08:00) 2017-09-06 18:10:28

  Maonesho ya mwaka 2017 ya China na nchi za kiarabu yamefunguliwa leo mjini Yinchuan, China. Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi, akisema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani zikiwemo nchi za kiarabu, kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja" ili kuhimiza amani na kunufaishwa kwa pamoja.

  Kwa niaba ya serikali na wananchi wa China, rais Xi amepongeza ufunguzi wa maonesho ya mwaka 2017 ya China na nchi za kiarabu, na kuwakaribisha watu wanaoshiriki kwenye maonesho hayo wakiwemo viongozi au wawakilishi wa nchi mbalimbali, wanaviwanda na wafanyabiashara na wasomi.

  Rais Xi amesema China ni rafiki na mwenzi mkubwa wa nchi za kiarabu. Wakati uchumi wa dunia unapofungamana siku hadi siku, ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili ambazo ni wenzi muhimu wa ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja" unapanuliwa na kupata mafanikio makubwa. Kwenye mkutano mkuu wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda mmoja na Njia moja" uliofanyika mwezi Mei mwaka huu, pendekezo lililotolewa na rais Xi la kujenga "Ukanda mmoja, Njia moja" iwe njia ya amani, ustawi, ufunguzi mlango, uvumbuzi na utamaduni lilikubaliwa na kuungwa mkono na nchi za kiarabu. Maonesho hayo ambayo kauli mbiu yake ni mambo halisi, uvumbuzi, ushirikiano na mafanikio ya pamoja yanafuata wazo la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda mmoja, Njia moja", na kujenga jukwaa muhimu kwa ajili ya kupanua ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu.

  Naibu spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Ping amesema, nchi za kiarabu ni washiriki na wajenzi muhimu wa pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja", anatumai kuwa China na nchi hizo zitaimarisha uratibu wa mkakati wa kujiendeleza, kuongeza biashara, kupanua ushirikiano katika mambo ya uwekezaji na fedha, na kuongeza ushirikiano wa nishati na maliasili.

  "Kukuza ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu kwa kufuata pendekezo la'Ukanda mmoja, Njia moja'kunalingana na mkondo wa hali ya sasa, utaratibu wa maendeleo na maslahi ya pande zote, na kuna mustakabali mzuri. China inapenda kushirikiana na nchi za kiarabu kufuata desturi ya kirafiki, kushikilia kanuni ya kujadiliana, kujenga na kunufaishwa kwa pamoja, na kusukuma mbele ujenzi wa'Ukanda mmoja, Njia moja'".

  Zikiwa wenzi wa jadi wa ushirikiano wa ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja", China na nchi za kiarabu zina historia ndefu ya kushirikiana kibiashara. China ni mwezi mkubwa zaidi wa biashara wa nchi za kiarabu. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2016, thamani ya biashara kati ya China na nchi za kiarabu ilizidi dola za kimarekani bilioni 171. Naibu spika wa bunge la Mauritania Bw. Mohammad Harshi alipohutubia ufunguzi wa maonesho hayo amesema,

  "Maonesho ya China na nchi za kiarabu yamekuwa mfano mzuri kwa ushirikiano wa uchumi kati ya pande hizo mbili na hata kati ya China na Afrika. Kutokana na maonesho hayo, ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Mauritania umekua, huku thamani ya biashara kati ya nchi hizo ikiongezeka siku hadi siku. Naamini maonesho hayo yataleta fursa nyingi zaidi kwa ajili ya ushirikiano wetu. Pia natumai watu wa uchumi na biashara wa nchi zetu watapnua zaidi ushirikiano kati yetu, ili kupata mafanikio makubwa zaidi"

  Kwenye maonesho hayo ya siku nne, makongamano kuhusu reli ya kasi, teknolojia, uchukuzi wa kimataifa, sheria za biashara, uwezo wa uzalishaji na kilimo yatafanyika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako