• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio la kuweka viwakzo dhidi ya wanaokwamisha mchakato wa amani nchini Mali

    (GMT+08:00) 2017-09-06 18:59:47

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio namba 2374 na kuamua kuweka vikwazo vya marufuku ya safari na kuganda mali za watu na mashirika yanayokwamisha mchakato wa amani nchini Mali.

    Azimio hilo limeeleza kuwa, watu na mashirika yatakayowekewa vikwazo yataamuliwa na kamati itakayoundwa kusimamia utekelezaji wa vikwazo hivyo. Baraza hilo linawataka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuwazuia watu wanaowekewa vikwazo kuingia au kupita nchi hizo, na kuganda mali za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja za watu na mashirika yanayowekwa vikwazo. Hatua za marufuku ya safari na kuganda mali zitaanza kutekelezwa ndani mwaka mmoja tangu azimio hilo kupitishwa.

    Azimio hilo pia linamtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuunda kikundi cha wataalamu, kusaidia kamati ya vikwazo kutekeleza jukumu hilo, huku likiutaka ujumbe wa Umoja huo nchini Mali MINUSMA kutoa msaada na kubadilishana habari na kamati ya vikwazo na kikundi cha wataalamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako